Monday, October 20, 2014

Waliokuwa wanandoa, Mariah Carey na mchekeshaji Nick Cannon wanaripotiwa kugombea mbwa wao nane wanaowachukulia kama marafiki.

Kwa mujbu wa gazeti la Sunday Express, ugonvi wa Mariah Carey na Nick Cannon umehamia kwenye mbwa wao nane waliokuwa wanaishi nao huku kila mmoja akitaka kuwa mmiliki na mwangalizi halali baada ya kuachana.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa wawili hao wamemaliza mgogoro wa £325 Million kwa makubaliano maalum.

Mariah na Nick Cannon walitengana mwezi Augus mwaka ikiwa ni miaka kadhaa tangu walipofunga ndoa mwaka 2008.

Hivi sasa Nick Cannon amejikita zaidi katika kazi yake huku akiendelea na kazi mpya ya kummeneji Amber Rose.

Inaelezwa kuwa hivi sasa Mariah Carey anaonekana kuwa kupitia kipindi kigumu na kwamba amenyong’onyea baada ya kuachana na mumewe huyo

Tumekuwa tukipata taarifa zinazohusu matukio ya mauaji ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara nchini Tanzania, hali ambayo imeonekana kukithiri katika siku za usoni huku jeshi la polisi likitoa ahadi ya kufanya jitihada za kuhakikisha linawatia nguvuni wahusika wa matukio hayo.

Taarifa iliyonifikia hivi punde kupitia Radio One Breaking News inahusu kuuawa kwa mtuhumiwa namba moja wa kesi ya ulipuaji mabomu jijini Arusha, Yahaya Hassan Omar kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi la polisi wakati alipojaribu kutoroka akiwa chini ya ulinzi.


MSANII nyota wa muziki wa Bongo Flava nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ huenda akaingia matatani baada ya juzi kupanda jukwaani kutumbuiza katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 akiwa amevaa sare ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), kinyume cha sheria.

Tangu msanii huyo afanye hivyo, mjadala umeibuka kwa wengi wao kujiuliza nini maana yake na kama alifanya hivyo kwa kibali maalumu au la, hasa ikizingatiwa ni hivi karibuni Jeshi hilo lilitoa onyo kwa wasanii na wengineo kutotumia mavazi hayo.

Mbali ya Diamond, hata vijana wake nao walishambulia jukwaa wakiwa katika mavazi hayo, akiwemo msanii aliyemshirikisha katika moja ya nyimbo zake, Ney wa Mitego.

Wakati shoo hiyo ikiendelea, baadhi ya mashabiki walianza kumzomea kila alipoimba kabla ya video kubwa ambazo zilikuwa mbele ya jukwaa hilo kuanza kuonyesha picha za mnato na video za mwanamuziki huyo akiwa amevaa mavazi hayo huku akiwa kama askari ‘anayekoki’ risasi katika katika bastora na baadaye katika bunduki ya kivita.

Kitendo hicho, kilionekama kuwakera zaidi maelfu ya wapenzi na mashabiki wa muziki waliokuwa wamejazana katika viwanja vya Leaders Club, huku kila mmoja akiwa na tafsiri yake.

Baada ya tukio hilo la juzi usiku, kitendo cha nyota huyo kuvalia mavazi hayo ya JWTZ, kimeibua mjadala hadi katika mitandao ya kijamii kuanzia jana asubuhi, ambapo picha za msanii huyo zikitumika kujenga hoja ya uhalali wa kufanya hivyo, huku vijana kadhaa wanaokutwa nazo mitaani wakiteswa vibaya na jeshi hilo.

Kwa upande wake Diamond, alitoa taarifa ndefu katika ukurasa wake wa Facebook na Instagram, akiishia kuelezea ni kwa nini alizomewa katika shoo hiyo.

Tanzania Daima ilipomtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura juu ya kitendo cha msanii huyo, alisema alikuwa hajui chochote na kuahidi kulifanyia kazi kama atapelekewa taarifa na wasaidizi wake.

Alipotafutwa Kaimu Msemaji wa JWTZ, Meja Joseph Msanja, simu yake iliita bila kupokelewa na alipotafutwa msaidizi wake, alikiri kupata taarifa na kujionea kupitia shoo hiyo, huku akisisitiza bosi wake anaweza kulizungumzia hilo.

Tukio hilo limefanyika ikiwa ni siku chache tu tangu kijana mmoja aliyekuwa amevalia mavazi ya kijeshi maeneo ya Kariakoo, jijini Dar es Salaam, kuvuliwa na kupewa adhabu ya kuogelea katika dimbwi la maji machafu yaliyotuama.

Aidha, msanii Gwamaka Kaihula ‘Crazy GK’ aliwahi kuhojiwa na Jeshi hilo kwa kutumia mavazi ya kijeshi katika kibao chake cha Simba wa Afrika, ambapo alijitetea pamoja na kuomba msamaha kwa kilichofanyika.

Kutokana na wimbi la watu mbalimbali hasa wasanii kuvalia mavazi yanayofanana na sare za jeshi hilo, hivi karibuni Kurugenzi ya Habari na Uhusiano Makao Makuu ya JWTZ, ilionya kama ifuatavyo:

Kumejitokeza kama fasheni kwa baadhi ya wasanii, hasa wanamuziki wa Bongo fleva, kurekodi video zao wakiwa wamevaa sare za jeshi kama vile suruali, viatu, fulana, kaptula, mabegi au kofia.


Inawezekana kwa namna moja ama nyingine, baadhi ya watumiaji wa sare hizo hawafahamu ni kinyume cha sheria ya nchi kukutwa nazo, ingawa kutokujua sheria bado sio utetezi mbele ya mahakama.

Mtu yeyote yule asiye na ruhusa ya kushona, kuuza au kuingiza nchini sare za jeshi, atakuwa ametenda kosa, kwa hiyo atafikishwa mahakamani na kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria zilizopo.

Katika uvaaji au uingizaji nguo, kama itatokea kwamba nguo hizo zinafanana kwa aina yoyote ile na zile za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, ikadhaniwa kuwa ni hizo, mtu huyo ana hatia na anastahili kufikishwa mahakamani na kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria zinazohusu sare za majeshi zilizopo


ilifafanua taarifa hiyo.

SOMO! Staa wa Bongo Movies, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ ameibuka na kumtaka msanii mwenzake, Blandina Chagula ‘Johari’ kukubaliana na matokeo ya aliyekuwa mpenzi wake Vincent Kigos ‘Ray’ kwamba kwa sasa ana uhusiano na mtu mwingine.

Staa wa Bongo Movies, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’.

Akistorisha na paparazi wetu, Aunty Lulu alimtaka Johari kukubaliana na matokeo na aige mfano wake kwani aliachana na Bond Bin Sinan ambaye kwa sasa ana mpenzi mwingine hivyo asimchukie Chuchu Hans anayetoka na Ray kwa sasa kwani kuachana ni jambo la kawaida katika mapenzi hivyo hatakiwi kuwa na kinyongo.

Msanii Bongo Movies, Blandina Chagula ‘Johari’.

“Mimi nimepitia kwenye maisha hayo ndiyo maana namshauri Johari akubaliane na matokeo kwamba Ray kwa sasa yupo na Chuchu Hans na asiwe na kinyongo naye ampende na aongee naye vizuri tu kwani ndiyo maisha,” alisema Aunty Lulu.

Mshtuko! Siku chache baada ya kujiengua kwenye nafasi ya uenyekiti katika Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ anadaiwa kufutwa uanachama wa klabu hiyo.

Aliyekuwa mwenyekiti katika Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.

Chanzo cha ndani ya klabu hiyo kimepenyeza madai kuwa, wameamua kumvua uanachama Steve kwani wanaona ni ‘kirusi’ ndani ya klabu kutokana na mwenendo wake.

“Steve amekuwa akiwashawishi baadhi ya memba wajiunge na upande wake, tofauti na umoja wa Bongo Movie Unity, viongozi wameamua kumfuta kabisa uanachama,” kilisema chanzo na kuongeza:
“Amewatangazia wenzake vibaya juzikati alivyokwenda Dodoma kwenye sherehe za kukabidhiwa kwa Rasimu ya Katiba Iliyopendekezwa kwa kuwaambia viongozi wa serikali kwamba wasanii ambao hawakwenda mjini humo ni Ukawa wakati si kweli.”

Katibu wa Bongo Movie Unity,William Mtitu akiwa ndani ya Ofisi za Global.

Baada ya chanzo chetu kujiridhisha na data hizo za ndani, mwanahabari wetu alimtafuta Steve Nyerere ili kujua anazungumziaje juu ya ishu hiyo ya kuenguliwa klabuni na mtazamo kuhusu suala hilo, alipopatikana alikuwa na haya ya kusema:

“Mimi ni mwanachana wa Bongo Muvi kama nimefutwa sijui lakini ni mwanachama. Kuhusu kuwasemea nilipokuwa Dodoma, ningewasemea mimi kama nani? Sina cheo cha kuwasemea wenzangu.
Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na tafrani kubwa Bongo Muvi huku madai mengi yakielekezwa kwa Steve.


NDOA basi! Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ amezima ndoto za kuishi maisha ya mke na mume kwa kudai kuwa, amebaini kujiingiza kwenye ulimwengu huo ni kujipa ‘stress’ za kujitakia.

Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda juzi, Dida alisema baada ya kuachana na aliyekuwa mume wake, Edzen Jumanne, amebaini wanaume wote lao ni moja hivyo kama atakubali kuingia kwenye ndoa na mwanaume mwingine, itakuwa ni yaleyale.

“Yani sasa hivi hata aje mwanaume na gia gani siwezi kukubali kuolewa tena, kwa kifupi sina ndoto za kuitwa mke wa mtu tena, bora nibaki peke yangu nifanye mambo yangu,” alisema Dida.